Skip to content
Scan a barcode
Scan
Paperback Weka Pesa Pata Pesa: Mashairi yanayohusu kamari na mengineyo [Afrikaans] Book

ISBN: B08J5CQ566

ISBN13: 9798618392709

Weka Pesa Pata Pesa: Mashairi yanayohusu kamari na mengineyo [Afrikaans]

'Weka Pesa Pata Pesa, ' hivyo ndivyo wachezesha kamari wanavyowashawishi na kuwadanganya watu wanaopenda kubeti ili kupata Pesa za bwerere!Vijana walio wengi pamoja na wazee wamejikuta kwenye uraibu wa kucheza kamari huku kila siku wakizidi kufilisika mali zao kutokana na michezo hiyo ya kubeti (kamari).

Ajabu kubwa ni pale unapowakuta vijana wanabeti au kucheza kamari tangu jua kuchomoza hata kuzama. Nani atalijenga taifa ikiwa nguvu kazi imezama kwenye uraibu wa kubeti? Pamoja na hayo, kitabu hiki pia kimesheheni mashairi mengine yanayohekimisha kuhusu maudhui tofauti tofauti. Karibu ujisomee kitabu hiki cha mashairi, ujihekimishe kupitia maneno kuntu yaliyotumika.

WASIFU WA MWANDISHI.
Mniko Chacha ni mwandishi wa vitabu vitano ambavyo ni Kiraka cha Ukombozi, Weka Pesa Pata Pesa, Songs of African Fathers, An Enemy of the Villagers, na Storms and Pleasures. Vitabu vyote hivi vinapatikana kwenye tovuti ya Amazon.

Mwaka huu, 2022 atachapisha riwaya yake mpya itakayojulikana kwa jina la 'Nitalipa Mahari na kuoa.'

Recommended

Format: Paperback

Condition: New

$9.21
Ships within 2-3 days
Save to List

Related Subjects

Poetry

Customer Reviews

0 rating
Copyright © 2026 Thriftbooks.com Terms of Use | Privacy Policy | Do Not Sell/Share My Personal Information | Cookie Policy | Cookie Preferences | Accessibility Statement
ThriftBooks® and the ThriftBooks® logo are registered trademarks of Thrift Books Global, LLC
GoDaddy Verified and Secured