Skip to content
Scan a barcode
Scan
Paperback Uchu Na Utamu Wa Kutawala Kwa Mabavu [Swahili] Book

ISBN: 1979653194

ISBN13: 9781979653190

Uchu Na Utamu Wa Kutawala Kwa Mabavu [Swahili]

Uchu na Utamu wa Kutawala kwa Mabavu ni kitabu cha historia kinachoeleza namna viongozi wa Tanganyika na Zanzibar na Afrika kwa jumla walivyotawala kwa mkono wa chuma. Mwandishi anaanza kwa kufafanua chanzo cha udikteta katika bara la Afrika, kushamiri kwa mfumo wa utawala wa chama kimoja na kujitokeza kwa mtindo wa kupindua serikali pamoja na vita vya wenyewe kwa wenyewe. Moja katika athari kubwa za mifumo hii ya kimabavu ni kusababisha wananchi wengi kukimbia na kuhama nchi zao na kutokomea ughaibuni kunusuru roho zao. Chini ya utawala wa mabavu umma huishi katika mateso na khofu kubwa katika nchi walizozaliwa bila ya kuwa na matumaini yoyote yale. Ustaadh Hashil Seif Hashil, mwandishi wa kitabu hiki, anaeleza pia kuhusu historia ya ukoloni ya Afrika Mashariki, biashara ya utumwa, siasa ya ukaburu, ukoloni mambo ya leo, ubeberu na kuimurika historia ilivyojaa uongo mwingi ulioandaliwa na wanahistoria Wazungu na wa nchi za Ulaya/Magharibi. Anapendekeza pia njia za kuondoa ufisadi na kurakibisha mambo katika nchi za Afrika na kuleta amani ya kudumu na maendeleo ya kisasa. Kitabu hiki kinastahiki kusomwa na wote, wazee na vijana, wasomi na walalahoi. Hii ni historia halisi ya Afrika Mashariki kwa ufupi ambako Mapambano Bado Yanaendelea.

Recommended

Format: Paperback

Condition: New

$8.97
50 Available
Ships within 2-3 days

Customer Reviews

0 rating
Copyright © 2025 Thriftbooks.com Terms of Use | Privacy Policy | Do Not Sell/Share My Personal Information | Cookie Policy | Cookie Preferences | Accessibility Statement
ThriftBooks ® and the ThriftBooks ® logo are registered trademarks of Thrift Books Global, LLC
GoDaddy Verified and Secured