Sudi na Shada pamoja na wenzao wamo darasani wanasoma kuhusu
aina za rangi. Shada anawauliza wenzake swali kutaka kujua kama
wanayaelewa mazingira ya darasani mwao. Je, swali hili linahusu nini?
Wanafunzi wanapata jibu lake ama wanashindwa?
Hadithi Mufti za Longhorn ni mfululizo mpya wa hadithi ambazo
zimeandikwa kulingana na mtaala mpya. Hizi hadithi zinalenga kukuza
ujuzi wa wanafunzi kupitia kwa uvumbuzi wa maarifa na zinaimarisha
uelewa wao wa masuala ibuka katika jamii. Hadithi hizi si tu za kuelimisha
na kuburudisha, bali pia zimeambatanishwa na mazoezi ambayo
yatawasaidia wanafunzi kuimarika kiubunifu, kimawazo na kifikra.