Mayalla ni wakili mashuhuri lakini amezungukwa na jamii iliyomkaba kama ukono. Yeye angependa kuishi safi safina lakini wakubwa wake kazini, wadogo wake, mkewe na hata abiria anaosafiri pamoja nao katika daladala moja wana tofauti naye, wote ni kama kaniki. Hawabadiliki na kutenda hata chembe ya uadilifu. Ni waovu kinehe! Si maadili katika ndoa, si biashara, si maamuzi ya mahakamani; yote ni hali moja, tenge...