Waswahili husema fani ya ujinga mwingi na elimu ni taa, gizani huzagaa. Je, iwapo mtu hajapata elimu ya vitabu wala ya maisha huwa mtu wa sampuli gani? Basi zamani za kale kulikuwa na ghulamu jina lake Fikirini. Elimu ya darasani hakuiona wala kuihisi. Alipata mke, Bi Halineshi, ingawa hakujua kumtunza kutokana na ujeuri na kiburi. Alimpa mkewe talaka bila kujua hamadi kibindoni silaha iliyo mkononi. Kwa talaka hiyo Bi Halineshi alimpata mchumba akamuoa kwani riziki haigombi. Je, Fikirini ataishi maisha gani bila elimu wala mke?