Skip to content
Scan a barcode
Scan
Paperback N'Na Kwetu: Sauti ya Mgeni Ugenini [Swahili] Book

ISBN: 1470942895

ISBN13: 9781470942892

N'Na Kwetu: Sauti ya Mgeni Ugenini [Swahili]

DIWANI hii ya N'na Kwetu: Sauti ya Mgeni Ugenini ilishinda kwenye awamu ya kwanza ya Tuzo za Fasihi ya Afrika kwa Lugha ya Kiswahili inayotolewa na Wakfu wa Mabati-Cornell mwaka 2015. Tungo nyingi zilizomo humu ziliandikwa baina ya robo ya mwisho ya mwaka 2010 na nusu ya mwanzo ya mwaka 2015. Hii ni miaka mitano ya mwanzo ya mshairi kuhamia na kuishi nchini Ujerumani - mbali na nyumbani kwao, Zanzibar. Ndani yake, kwa hivyo, muna muakisiko wa hisia za mgeni ugenini, akitayamani mengi mazuri ya kwao na akijutia kuyaacha nyuma yake. Ukweli ni kuwa wakati mtu anapoishi ugenini, ndipo hasa ile thamani ya kwao anapoitambua na kutaka kujitambulisha nayo zaidi na zaidi. Ndipo hisia za kutambuwa kuwa ana kwao zinapopanda kiwango cha juu. Kutoka kipembe cha mbali, Mohammed Ghassanani anakuangalia kwao na kuyaona mambo ambayo alipokuwamo ndani yake, alikuwa hata hajui kama yapo. Chembilecho Wajapani: "Samaki hajijui kuwa amerowa!" Na sababu ya kutokujijuwa huko, kwa hakika, ni kwa kuwa yeye mwenyewe anaishi ndani ya maji muda wote.

Recommended

Format: Paperback

Condition: New

$18.29
Ships within 2-3 days
Save to List

Customer Reviews

0 rating
Copyright © 2026 Thriftbooks.com Terms of Use | Privacy Policy | Do Not Sell/Share My Personal Information | Cookie Policy | Cookie Preferences | Accessibility Statement
ThriftBooks® and the ThriftBooks® logo are registered trademarks of Thrift Books Global, LLC
GoDaddy Verified and Secured