Skip to content
Scan a barcode
Scan
Paperback Nasikia Sauti ya Mama [Swahili] Book

ISBN: 9966312757

ISBN13: 9789966312754

Nasikia Sauti ya Mama [Swahili]

Ken Walibora ni miongoni mwa waandishi arifu na maarufu

zaidi wa fasihi ya Kiswahili waliowahi kuibuka katika Afrika

Mashariki na ya Kati. Mbinu ya kalamu yake ina mvuto

mkubwa na uzuri wa kisanaa wa aina yake. Ameziandika tanzu

mbalimbali za fasihi kama vile riwaya, ushairi na tamthilia.

Hata hivyo, Nasikia Sauti ya Mama ndiyo kazi yake ya

kwanza inayostahili kuitwa tawasifu, tawasifu inayoangazia

kipande kidogo halisi cha maisha yake mwenyewe na wala si

ya wahusika wake ambao ni zao la ubunifu.


Nasikia Sauti ya Mama ni tawasifu iliyosheheni mtindo wa

usimulizi wenye uwazi, ujasiri na umbuji. Uzuri wa kisanaa wa

tawasifu hii unashadidia ukweli usiokanushika kwamba

mwandishi huyu, aliyeibuka kwanza na riwaya ya Siku Njema,

ataendelea kutamba kwa miaka na mikaka katika medani ya

fasihi ya Kiswahili.

Recommended

Format: Paperback

Temporarily Unavailable

We receive fewer than 1 copy every 6 months.

Save to List

Related Subjects

Fiction Literature & Fiction

Customer Reviews

0 rating
Copyright © 2026 Thriftbooks.com Terms of Use | Privacy Policy | Do Not Sell/Share My Personal Information | Cookie Policy | Cookie Preferences | Accessibility Statement
ThriftBooks® and the ThriftBooks® logo are registered trademarks of Thrift Books Global, LLC
GoDaddy Verified and Secured