Hadithi za Bibilia katika kitabu hiki cha picha zitawasaidia watoto kukumbuka kwamba haijalishi yoyote yanayofanyika katika maisha yao ama yaliyowazingira, Mungu anawajali na anawaangalia usiku na mchana. Tofauti na wazazi, Mungu halali wala kuchoka. Mungu pia yuajua yatakayofanyika. Ni mwaminifu na hutimiza ahadi zake.