MWANA-ADAM NI NANI NAYE NI NINI MUNGU AMKOMBOE (MNNNMA), kimeandikwa kuufikia umma wote wa wanao zungumza Kiswahili tulio tumwa kwao. Pia kimechapishwa katika vijitabu vidogo tokea baadhi ya masomo yake. Kwa uelewa huu basi, kama mpendwa unacho kimoja wapo ya hivi, tambua kwamba huo siyo ujumbe wote unao kustahili kuupokea. Tunasema hivi sababu kitabu MNNNMA kimegawanyika katika vyuo vitatu vikupasavyo mpendwa kuhitimu: CHUO CHA KWANZA hufunza kuhusu Mwanzo Mtakatifu & Kuingia Dhambi. CHUO CHA PILI hufunza kuhusu Fumbo La Ukombozi & Ufunuo wa Ukombozi. CHUO CHA TATU hufunza kuhusu Mwisho Mtakatifu & Kuondoka Dhambi. Hivyo ni ushauri wetu umiliki kitabu chote cha (1) MWANA-ADAM NI NANI NAYE NI NINI MUNGU AMKOMBOE. Lakini kama hivyo sivyo kwako, basi uanze na (2) CHUO CHA KWANZA, ndipo kifuatie (3) CHUO CHA PILI, na ndipo umalizie na (4) CHUO CHA TATU. Na kama hata hivi sivyo ilivyo kwako, basi acha tukuvutie kwa baadhi ya masomo ndani ya MNNNMA tuliyo yatoa kama vitabu huria: (5) Historia na Maisha ya Yeshua Kristo, (6) Jinsi ya Kusali & Kuongea na YAHWEH, (7) Utatu Mtakatifu, (8) Mafundisho ya Utajiri, (9) Mafundisho ya Ndoa, (10) Ufufuo na Uchukuo, (11) Yisrael, (12) Ujio wa Pili wa Yeshua Kristo. Ni lengo letu kitabu cha Milenia ya Kristo kisambazwe bure katika masoko ya vitabu mitandaoni. Lengo lake hiki ni kuitambulisha kazi ya MNNNMA kwao wote wanaoishi ughaibuni, lakini wanaongea Kiswahili. Kwa jinsi hii, hawa pia wapokee ujumbe wao, kupitia umiliki wa kitabu MNNNMA. Kitabu hiki MNNNMA kinaleta habari njema kwa kanisa zima linalo zungumza Kiswahili. Kitabu chako hiki kinaifumbua hadithi ya fumbo la nyakati, na pamoja nalo hilo, kinategua kile kitendawili cha kale, pale malaika walipo muuliza Mungu: ... Je mtu (anaye kufa) ni nini, ambaye wewe unamjali hivi? Na mwana wa adam, ambaye wewe humtembele? ... [Zaburi 8:4-6]. Ni ndani ya fumbo hilo la nyakati, na uteguzi wa kitendawili hicho, ndimo historia yote ya mtu na ukombozi wake vilihifadhiwa kwa umahiri na umakini usio pimika.
ThriftBooks sells millions of used books at the lowest
everyday prices. We personally assess every book's quality and offer rare, out-of-print treasures. We
deliver the joy of reading in recyclable packaging with free standard shipping on US orders over $15.
ThriftBooks.com. Read more. Spend less.