Skip to content
Scan a barcode
Scan
Paperback Mbali an Nyumbani [Swahili] Book

ISBN: 9966364544

ISBN13: 9789966364548

Mbali an Nyumbani

Mbali na Nyumbani ni riwaya ya kitawasifu inayosimulia ari ya

mhusika mkuu ya kukisaka ikipendacho roho. Ukosapo mapenzi

utaondoka nyumbani uende mbali ukayasake; ukosapo masomo

utafanya vivyo hivyo. Ukosapo mara ki au kazi utajipata barabarani

ukitamba na njia kwenda kuisaka. Je, unaposukumwa na ari au

utundu wa kitoto utaenda mbali na nyumbani kuukomesha

utundu huo na kuizima kiu ya kujua usiyoyajua? Kama ni kutafuta

maarifa, hiyo ni heri... mpaka safari igeukapo kuwa na shari ndipo

utakapobaini ukweli kwamba nyumbani hamna mfanowe hata

pawe ni pangoni.

Adam Sha katika maisha ya kiuhalisia anatoka nyumbani kwao

Zanzibar akiwa amefumwa na mkuki wa kiu ya elimu. Anapo ka

Bungoma anaselelea. Anafanya yote ya kufanywa na kijana wa

rika lake. Kisha anatumia ujanja wake kuvuka mpaka na akajipata

nchini Uganda. Anapo ka Khartoum karibu tamaa ya kuendelea

na safari inamwondokea. Kula ni kwa nadra na kulala ni taabu

tupu. Hatimaye anajipata Kairo. Anaporudi Zanzibar, nyumbani

hapamweki. Mara hii anajipata Ujerumani kwa ufadhili wa kisiasa,

ambako nako pia panamkataa. Kisa na maana?

Mbali na Nyumbani ni kisa cha matukio halisi lakini chenye msuko

wa kiriwaya na chenye sifa zote za riwaya.

Recommended

Format: Paperback

Temporarily Unavailable

We receive fewer than 1 copy every 6 months.

Related Subjects

Fiction Literature & Fiction

Customer Reviews

0 rating
Copyright © 2025 Thriftbooks.com Terms of Use | Privacy Policy | Do Not Sell/Share My Personal Information | Cookie Policy | Cookie Preferences | Accessibility Statement
ThriftBooks ® and the ThriftBooks ® logo are registered trademarks of Thrift Books Global, LLC
GoDaddy Verified and Secured