"MAISHA YANGU: KHAINI AU MUHANGA WA MAPINDUZI YA ZANZIBAR?" ni kitabu kinachoeleza historia ya Zanzibar ya hivi karibuni na vipi Muungano baina ya Zanzibar na Tanganyika ulivyoanzishwa hadi kuwepo taifa jipya la TANZANIA. Khamis Abdulla Ameir amejaribu kwa kadri ya uwezo wake kuweka sawa historia ya Muungano wa Tanzania katika njia iliokuwa sahihi kabisa, ili Watanzania wa leo na wa vizazi vijavyo, waweze kuelewa chanzo na malengo halisi ya Muungano huu. Kitabu hiki kinasimulia historia mpya ya kileo kuhusu vipi vyama vya siasa vilivyoanzishwa Zanzibar katika mwaka 1957 na vipi vyama hivyo na vyama vya wafanyakazi vilivyodai uhuru wa Zanzibar kutoka kwa Balozi Mkaazi wa Uingereza na sio kutoka kwa Mfalme Mwarabu ambaye alikuwa hana sauti mbele ya Balozi wa Uingereza. Zanzibar ilipata uhuru wake tarehe 10 Disemba, 1963 na serikali ya mseto ya ZNP/ZPPP ikakabidhiwa madaraka baada ya kushinda katika uchaguzi. Mwandishi anaeleza vipi Mapinduzi ya Zanzibar yalivyotekwa nyara na Mabeberu wa Uingereza na Marekani kwa kushirikiana na Viongozi wakuu wa Kenya, Uganda na Tanganyika ili Zanzibar isiweze kutekeleza siasa ya Kisoshalisti, ambayo nchi hiyo ilishaanza kuitekeleza kivitendo. Frank Carlucci, jasusi maarufu wa CIA, alipelekwa Zazibar na serikali yake kwa kazi moja tu, nayo ni kuizuia Zanzibar isijekuwa CUBA YA AFRIKA na kuziambukiza siasa ya Usoshalisti nchi jirani za Afrika Mashariki na Afrika kwa jumla. Kitabu kilichapishwa na DL2A Buluu Publishing, jijini Paris, Ufaransa.
Format:Paperback
Language:Swahili
ISBN:B09TZCV6F8
ISBN13:9791092789096
Release Date:March 2022
Publisher:Diffusion Des Litteratures En Langues Africai
ThriftBooks sells millions of used books at the lowest everyday prices. We personally assess every book's quality and offer rare, out-of-print treasures. We deliver the joy of reading in recyclable packaging with free standard shipping on US orders over $15. ThriftBooks.com. Read more. Spend less.