Dhuluma za kijinsia ni za namna nyingi. Wanawake wanadhulumiwa katika vipengele mbalimbali vya maisha. Wanadhulumiwa katika ndoa, katika mazingira ya kazi, katika uwanja siasa na katika taasisi na shughuli za kidini. Na si hivyo tu. Wanadhulumiwa kimwili na qwenzao wa kiume; wanapokamatwa na kupelekwa kwenye cvituo vya polisi; au wanapotafuta huduma za kiserikali. Dhuluma za kimwili dhidi ya wasichana ambazo zinazungumziwa kwa m, inong'ono ni zile za baba kwa binti zao. Dhuluma hizo zipotokea watu ushauriwa wanyamaze ili kulinda jina la familia inayohusika. Mchezo wa kwenzi Gizani unahusu baba aliyemdhuluma binti na binti ya binti huyo kukataa katakata kunyamazishwa. Aliamua kupigania haki ya binti yake kisheria licha ya kushauriwa na jamaa zake, waumini wa kanisa lake na wengineo kwamba suala hilo lishughulikiwa na kusuluhishwa kinyumbani.