Mama amepata mimba wakati kensa ya rushwa imeenea nchini. Hospitali huwezi ukatibiwa bila kutoa hongo; madereva hawajali sheria za barabara kwa sababu watahonga; shuleni hongo inaamua kama mtoto atachukuliwa au la. Kuna kinga yoyote ya uovu huu? Mtoto atazaliwa katika hali gani?