Kidole cha Habiba ni kimoja cha vitabu katika
msururu wa Little Birds ECDE vilivyoandikwa kuwapa
watoto maarifa na ujuzi wa kujilisha. Yanayofundishwa
katika hadithi hii ni pamoja na kunawa mikono kabla ya
kula na adabu njema wakati wa kula.
Lengo la msururu huu ni kuhimiza usomaji miongoni mwa
watoto. Msamiati uliotumiwa kuandika hadithi hizi ni rahisi na
wa kawaida. Picha na michoro maridadi na ya kupendeza
imetumiwa ambayo inaifanya hadithi iwe ya kupendeza na
kufurahisha. Hii itasaidia kuwachochea watoto kujadili
yaliyomo wanaposoma.