Skip to content
Scan a barcode
Scan
Paperback Kazi Za Christopher Mwashinga, Juzuu YA III: Mashairi Book

ISBN: B08CWM9RTN

ISBN13: 9798665080109

Kazi Za Christopher Mwashinga, Juzuu YA III: Mashairi

Mfululizo huu wa Kazi za Christopher Mwashinga una lengo la kuwafikia wasomaji wa lugha ya Kiswahili kila mahali lugha ya hiyo adhimu inapotumika. Christopher R. Mwashinga alianza kuandika kazi mbalimbali kwa lugha ya Kiswahili mwanzoni mwa miaka ya 1980. Toleo hili la mfululizo wa kazi zake za Kiswahili, linahusisha mashairi, barua na maandiko yake mengine, ikiwa ni pamoja na kazi zake za kisomi na kitaaluma zilizowahi kuchapishwa kwa Kiswahili katika vitabu, magazeti, na majarida mbalimbali. Aidha mradi huu unahusisha pia kazi zake zilizotafsiriwa toka lugha ya Kiingereza. Miongoni mwa mambo mengine, maandiko yake yaliyowekwa katika majuzuu haya yamehifadhi maarifa na historia ya muhimu inayoihusu jamii yote kwa ujumla, na kwa namna ya kipekee, jamii ya Kikristo, hasa katika ukanda wa Afrika Mashariki. Baadhi ya mambo yaliyomo katika majuzuu haya, hayajarekodiwa mahali pengine popote katika historia ya watu wa Afrika Mashariki. Ukweli huu unafanya mfululizo huu wa machapisho yake uwe wa muhimu sana katika kazi za wenyeji wa Bara la Afrika zilizochapishwa katika miongo ya hivi karibuni. Juzuu hii ya tatu inahusisha mashairi yake yaliyoandikwa katika miongo miwili ya kwanza ya karne ya ishirini na moja (2001-2020). Mashairi haya yaliandikwa katika mabara manne: Afrika, Asia, Amerika ya Kaskazini na Ulaya.

Recommended

Format: Paperback

Condition: New

$23.95
Ships within 2-3 days
Save to List

Related Subjects

Poetry

Customer Reviews

0 rating
Copyright © 2026 Thriftbooks.com Terms of Use | Privacy Policy | Do Not Sell/Share My Personal Information | Cookie Policy | Cookie Preferences | Accessibility Statement
ThriftBooks® and the ThriftBooks® logo are registered trademarks of Thrift Books Global, LLC
GoDaddy Verified and Secured