Fumo Liongo alikuwa shujaa wa mji wa Pate katika Pwani ya Afrika ya Mashariki aliyeishi kati ya karne ya 9 na 13.
Umaarufu wa Fumo Liongo ulitokana na ushujaa, uzalendo na kipaji chake cha umalenga miongoni mwa watu wa Pate na maeneo ya jirani. Kwa Mfalme Mringwari, ushujaa na umaarufu wa Liongo ni tishio kubwa dhidi ya utawala wake. Kilele cha hofu na chuki dhidi ya Fumo Liongo kinafikiwa pale Liongo anapoliongoza jeshi vitani na kuwashinda Wagala, maadui zao wa jadi. Licha ya kuitetea na kuilinda Pate dhidi ya wavamizi, Liongo hapati pongezi bali shukurani za punda kwani Mfalme Daudi Mringwari anapania aitoe roho yake. Anasema, "Nimelifuga joka hili tukutu ndani ya tundu la ufalme wangu ... ila sasa nitaliteketeza kwa moto,
niligeuze majivu baridi badala ya kulizika kiwiliwili."
Hakika ukianza kusoma hutaachia kitabu hiki hadi umejua mwisho wa kisa hiki cha kusisimua na cha kihistoria. Ni imani ya mwandishi na mchapishaji kuwa tamthilia hii itachochea fikira za wasomaji na kuzidi kutajirisha wapenzi wa lugha ya Kiswahili kwa vionjo na misamiati lukuki.
Profesa Emmanuel Mbogo ni Mwandishi nguli wa tamthilia, riwaya na hadithi fupi zenye maudhui ya kihistoria, kijamii na masuala mtambuko. Baadhi ya vitabu vyake ni: Giza Limeingia, Tone la Mwisho, Watoto Wetu, Morani, Ngoma ya Ng'wanamalundi, Sundiata, Ndoto za Josef, Vipuli vya Figo, Sadaka ya John Okelo, Watoto wa Mamantilie, Bustani ya Edeni, Mizungu ya Manabii, Tanzia ya Patrice Lumumba, Wachawi wa Bongo, Wangari Maathai, Nyota ya Tom Mboya, Malkia Bibi Titi Mohamed, Mtumwa hadi Siti Bint Saad na Mondlane & Samora.
Fumo Liongo was a warrior from the city of Pate on the East African coast who lived between the 9th and 13th centuries.
Fumo Liongo's fame stemmed from his bravery, patriotism and his talent for eloquence among the people of Pate and the surrounding areas. For King Mringwari, Liongo's bravery and fame are a major threat to his rule. The height of fear and hatred against Fumo Liongo is reached when Liongo leads an army into battle and defeats the Gala, their traditional enemies. Despite defending and protecting Pate from invaders, Liongo receives no praise but only the gratitude of donkeys as King Daudi Mringwari intends to take his life. He says, "I have tamed this mighty dragon in the den of my kingdom ... but now I will burn it with fire,
I will turn it into cold ashes instead of burying its body."
Once you start reading, you will definitely not put this book down until you know the end of this exciting and historical story. It is the author and publisher's belief that this play will stimulate the imagination of readers and further enrich Swahili language lovers with rich flavors and vocabularies.
Professor Emmanuel Mbogo is a prolific writer of plays, novels and short stories with historical, social and cross-cutting themes. Some of his books are: Giza Limeingia, Tone la Mwisho, Watoto Wetu, Morani, Ngoma ya Ng'wanamalundi, Sundiata, Ndoto za Josef, Vipuli vya Figo, Sadaka ya John Okelo, Watoto wa Mamantilie, Bustan ya Eden, Mizungu ya Manabii, Tanzia ya Patrice Lumumba, Wachawi wa Bongo, Wangari Maathai, Nyota ya Tom Mboya, Malkia Bibi Titi Mohamed, Mtumwa hadi Siti Bint Saad and Mondlane & Samora.