Skip to content
Scan a barcode
Scan
Paperback Bweni la Wasichana [Swahili] Book

ISBN: 9987753841

ISBN13: 9789987753840

Bweni la Wasichana [Swahili]

Usiku huo nilikuwa nasimamia maandalizi ya masomo ya usiku. Nikapigiwa simu na Rose, nikaipokea. Wakati naongea naye, nikawa natembea taratibu kama naelekea kwenye mabweni. Ghafla, nikaona taa za bweni wanalolala "Buibui" zinawaka na kuzima, nikajua ni hitilafu katika mfumo wa umeme. Nikataka kusogea ili nithibitishe kisha nitoe taarifa mapema kwa uongozi na matengenezo yafanyike. Nilisogea mpaka mlangoni, taa zikawaka moja kwa moja, na kwa kuwa kulikuwa na dalili za kuwemo mwanafunzi, nilitaka kujua kwanini hayupo darasani wakati wenzake wote walikuwa wana-jisomea. Nilingia nikakuta hali ya ukimya sana, nikatembea mpaka karibu na mwisho wa bweni, nilichokiona ni aibu kubwa Huwezi amini, "Buibui" waliponiona wakadondosha khanga Wakabaki kama walivyozaliwa..


LUCAS GERVAS LUBANGO ni mwalimu wa masomo ya biashara alivesoma Shule ya Sekondari ya Wavulana ya Kibaha (ECA). Elimu ya juu aliipata katika chuo kikuu cha Dares salaam, akisomea Shahada ya Ualimu katika Masomo ya Biashara. Bweni la Wasichana ni riwaya yake ya kwanza na imeshika nafasi ya pili kwenye Tuzo ya Safal Cornel.

Recommended

Format: Paperback

Condition: New

$28.88
Ships within 2-3 days
Save to List

Related Subjects

Fiction Literature & Fiction

Customer Reviews

0 rating
Copyright © 2026 Thriftbooks.com Terms of Use | Privacy Policy | Do Not Sell/Share My Personal Information | Cookie Policy | Cookie Preferences | Accessibility Statement
ThriftBooks ® and the ThriftBooks ® logo are registered trademarks of Thrift Books Global, LLC
GoDaddy Verified and Secured