Skip to content
Scan a barcode
Scan
Hardcover Barabara ya Tanzania Kwenda Damascus [Swahili] Book

ISBN: 8797435007

ISBN13: 9788797435007

Barabara ya Tanzania Kwenda Damascus [Swahili]

Baada ya Vita Vikuu kumalizika 1918 Ujerumani iliachia miliki zake za nje, ikiwemo miliki yake ya Afrika Mashariki, kwa umoja wa mataifa makuu na mamlaka-shiriki (Principal Allied and Associated Powers) yaliyoshinda vita. Kutokana na mabadiliko hayo, Uingereza ilikubali wajibu wa kimataifa wa kusimamia maendeleo ya kisiasa ya sehemu kubwa ya miliki ya Kijerumani ya Afrika Mashariki; ambayo baadaye iliitwa Jimbo la Tanganyika (Tanganyika Territory); hadi hapo wenyeji wa Jimbo wagekuwa tayari kujisimamia wenyewe. Kwa miongo minne, Uingereza ilitekeleza wajibu huo kulingana na uwezo wake hadi Jimbo lilipojitawala Desemba 9, 1961.


Usultani wa Zanzibar, ambao pia ulikuwa chini ya Waingereza ingawa kwa utaratibu mwingine, ulijitawala Desemba 10, 1963. Mwezi mmoja baadaye, Januari 12, 1964, yalitokea mapinduzi ya kimbari nchini humo yaliyoiondoa madarakani serikali mpya kwa nguvu na kufuta taasisi ya kisiasa na kijamii ya usultani wa kikatiba. Zanzibar na Tanganyika ziliungana Aprili 26 mwaka huo na hivyo kuwa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.


Lakini muungano huu siyo shwari, na misingi ya kiutawala iliyounda taifa jipya la Tanzania haikukidhi viwango vya kimataifa vinavyokubalika. Katika sehemu nne, kazi hii inajadili kilichojiri tangu utawala wa kigeni hadi kujitawala na pia kutathmini njia taifa hili iliyochukua kuelekea mabadiliko ya kisiasa, kijamii, kiuchumi, kimaendeleo na kiutamaduni.

Recommended

Format: Hardcover

Condition: New

$15.20
Save $2.79!
List Price $17.99
Ships within 2-3 days
Save to List

Related Subjects

Education Education & Reference

Customer Reviews

0 rating
Copyright © 2026 Thriftbooks.com Terms of Use | Privacy Policy | Do Not Sell/Share My Personal Information | Cookie Policy | Cookie Preferences | Accessibility Statement
ThriftBooks ® and the ThriftBooks ® logo are registered trademarks of Thrift Books Global, LLC
GoDaddy Verified and Secured